6/30/16

Mlowola, Dk Hosea watofautianaMkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola ametofautiana na mtangulizi wake, Dk Edward Hoseah kuhusu taasisi hiyo kupewa meno ya kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa rushwa, akisema ni busara kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuendelea na jukumu hilo.

Amesema kuna faida nyingi za DPP kufanya kazi ya kupitia majalada na kuwashtaki watuhumiwa, badala ya kazi hiyo yote kufanywa na Takukuru pekee, akisema mchakato huo husaidia kuondoa upungufu.

Dk Hoseah, ambaye aliondolewa kwenye wadhifa huo kwa maelezo kuwa alishindwa kuwajibika ipasavyo kwenye suala la wizi wa makontena, alikuwa akimshtumu DPP mara kwa mara kwa kuchelewesha kupeleka kesi mahakamani na kutaka Takukuru ipewe mamlaka ya kufikisha watuhumiwa mahakamani.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts