6/24/16

Msama amuomba radhi Dk Harrison MwakyembeSiku mbili baada ya Mhariri wa gazeti la Dira ya Mtanzania Mussa Mkama kupandishwa kizimbani kwa tuhuma ya kuchapisha habari yenye uchochezi, Kampuni ya Msama Promotion inayomiliki gazeti la Dira ya Mtanzania, imemsimamisha kazi mhariri huyo.


Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Harrison Mwakyembe kutokana na habari mbili zilizochapishwa na gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki.


Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Msama amesema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’, haikufuata misingi ya uandishi wa habari.


Aidha, Msama amesema hatua nyingine anayochukua ni ya kumsimamisha kazi mhariri huyo kwa madai kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi.


Amesema anamsimamisha kazi mhariri huyo na hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm