6/10/16

‘Mtoto wa Nyani’ adaiwa kubaka mwanafunzi

 
Baraka Joshua (23), inayedaiwa alikuwa akiishi na nyani baada ya kuzaliwa na kutupwa porini mkoani Shinyanga takriban miaka minane iliyopita,  amepandishwa kizimbani Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu mashtaka ya kumbaka na kumlawiti mtoto wa miaka tisa.
Alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Florida Wenceslaus. Alidai Mei 17 eneo la Shule ya Msingi Tabata Kimanga, mshtakiwa alitenda makosa hayo dhidi ya mtoto ambaye alikuwa anasoma katika shule hiyo.
Mshtakiwa huyo alikana mashtaka na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.  Hakimu Catherine Kiyoja aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 26, ikapotajwa tena.
Awali, mshtakiwa anadaiwa alikuwa anaishi na nyani kabla hajachukuliwa na askari wa wanyamapori baada ya kumfuatilia kwa karibu.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts