Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

6/28/16

Mtuhumiwa Mauji ya Mwangosi Akipatikana na Hatia Kunyongwa

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa imepanga kutoa hukumu ya kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Chanel 10 mkoani humo, Daudi Mwangosi, Julai 21, mwaka huu na endapo mtuhumiwa atapatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia atahukumiwa kunyongwa.Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili askari polisi, Pasificus Simon, anayetuhumiwa kufanya maujai hayo, Paulo Kihwelo, aliyasema hayo jana mara baada ya kusikiliza majumuisho na maoni ya wazee wa baraza wa mahakama hiyo.

Alisema ni wajibu wake kutoa majumuisho kwa kuangalia mazingira na ushahidi uliomgusa mtuhumiwa moja kwa moja.

Jaji Kihwelo alisema katika kesi hiyo, mtuhumiwa anadaiwa kuwa, Septemba 2, 2012 alimuuua Mwangosi kwa kukusudia na endapo Ikithibitika kutenda kosa hilo atapewa adhabu ya kifo.

Hata hivyo, alisema mwenye jukumu la kuthibitisha kosa kwa mtuhumiwa ni upande wa mashtaka ambao unatakiwa uthibitishe bila kuacha shaka yoyote kuwa alifanya hivyo na si upande wa mtuhumiwa kuthibitisha kuwa mtuhumiwa hajatenda kosa.

Jaji Kihwelo alitaja vielelezo ambavyo vilitolewa mahakamani bila kupigwa ni ramani ya tukio, taarifa ya uchunguzi ya kifo cha marehemu, ungamo la mtuhumiwa kwa mlinzi wa amani na kitabu cha kuchukilia silaha FFU cha Iringa.

Akisoma majumuhisho kwae upande wa ungam, alisema maungamo yanayofanywa mbele ya mlinzi wa amani yanaweza kutumika kutoa ushahidi.

Kwa upande wake, mtuhumiwa huyo alieleza mahakama wakati akitoa ushahidi wake kuwa, kabla ya kufika kwa mlinzi wa amani aliitwa kuhojiwa na RPC na RCO baadaye alienda kufanya ungamo kwa mlinzi wa amani ambako hakufanya chochote zaidi ya kutakiwa kusaini .

Alidai wakati akienda wa mlinzi wa amani alisindikizwa na Sajenti Erick ambaye alikuwa na bahasha ya khaki na alimkabidhi mlinzi huyo wa amani na kumueleza amepewa na RCO na baada ya kupokea alisoma na kuandika na baadaye alimpa aisaini.

Mmoja wa wazee wa baraza, Khadija Hussein, akitoa maoni yake, alisema kwa kuwasikiliza mashahidi wa pande zote kuanzia kesi ilipoanza hadi ilipofikia, amegundua kuwa mtuhumiwa alienda kufanya ungamo kwa mlinzi wa amani akiwa huru na kusaini.

Alisema siyo rahisi mtu kusaini kitu ambacho hajakitolea maelezo, hivyo alichokisaini ndicho alichokitenda kwani alitoa ungamo akiwa huru bila kupigwa wala kutishiwa na mtu yeyote.

Alisema endapo maelezo hayo yalikuwa siyo yake, yangepingwa mbele ya mahakama na wakili wake au yeye mwenyewe, lakini kwa kuwa yalipokelewa bila kupingwa hivyo anahatia ya kutenda kosa bila kukusudia.

Lakini mzee wa baraza wa pili, Said Mbaga, alisema mtuhumiwa hana hatia kwa sababu shahidi wa kwanza hakuthibitisha bila kuacha shaka mtuhumiwa kutenda kosa, kwa sababu hakumuamuru kupiga bomu na kati ya askari waliokuwa kwenye tukio hilo haijulikani nani aliyepiga.

Naye mzee wa baraza wa tatu, Sophia Ng’anguli, alisema mtuhumiwa alitenda kosa bila kukusudia licha ya upande wa mashtaka kuacha mashaka katika ushahidi wao.

Alidai kitu cha msingi kinachomfunga mshitakiwa ni ungamo lake alilolitoa kwa mlinzi wa amani, ambalo aliandika na kusaini huku akikiri na kujutia. Kesi hiyo ilikuwa ikiongozwa na mawakili wawili wa serikali, Wakili Mkuu wa Serikali, Sunday Hyera na Wakili Mwandamizi, Ladislaus Komanya, lakini jana wakati Jaji Kihwelo akitangaza kupanga hukumu ya kesi, ilikuwa ikiongozwa na Wakili wa Serikali Adolf Maganda na wakili wa utetezi Rwezaura Kaijage
 
CHANZO: NIPASHE