Mwakyembe apiga jeki mil. 5/- ujenzi wa vyoo vya shule | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/13/16

Mwakyembe apiga jeki mil. 5/- ujenzi wa vyoo vya shule
MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ametoa msaada wa Sh. milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo vya Shule ya Msingi Mpanda Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.


Msaada huo umekuja ikiwa ni siku chache baada ya gazeti la Nipashe kuibua kero ya wanafunzi 700 na walimu 16 wa shule hiyo kujisaidia katika choo kimoja chenye tundu moja na baadhi yao porini.

Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, alitoa msaada huo baada ya kutembelea shule hiyo kufuatia taarifa zilizochapishwa na gazeti hili siku chachezilizopita.

Mbali na Dk. Mwakyembe, wadau wengine wakiwamo waliosoma shuleni hapo waliopo mikoa mbalimbali na Marekani, tayari wameanza kukusanya michango ya fedha ili kuisaidia shule hiyo.

Michango hiyo inakusanywa na Meneja wa Kituo cha Redio Kyela, Maisha Ambangile.

Awali shule hiyo ilikuwa na choo chenye matundu 18, lakini kilibomoka kutokana na mafuriko.

Aidha, mafuriko hayo yaliyotokea Aprili, mwaka huu, yalisababisha madhara mbalimbali kwa wananchi na majengo ya taasi, hali iliyoilazimu Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kuzifunga shule 10 kwa lengo la kuwaepusha wanafunzi wasipate maafa.

google+

linkedin