6/2/16

Mwenyekiti amuokoa mbunge kwa madiwani
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Murshidi Ngeze amemuokoa Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza baada ya madiwani kumtaka afanye marekebisho kwenye Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (CDF).


Madiwani hao wamemtaka mbunge huyo kufumua bajeti ya mfuko, ili kupata fedha za ujenzi wa Daraja la Kyamabale, Kata ya Mikoni.


Hata hivyo, Rweikiza akizungumza kwa simu kutoka Dodoma, amesema daraja hilo lilikuwa limetengewa fedha zake za ujenzi ambazo zilitafunwa.


Diwani wa Nyakato, Daniel Damian amesema mkandarasi anahitaji Sh70 milioni ili aanze kazi, kuna upungufu wa milioni 26 hivyo ni bora zikatoka kwenye mfuko wa jimbo.


Ngeze amewaomba madiwani wasitangulize lawama kwa mbunge, bali ajulishwe kwanza kuhusu pendekezo hilo la kutaka mfuko huo kuchangia Sh26 milioni.

Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm