Nay wa Mitego adai ‘Free Nation 966’ itakuwa lebo tofauti na zingine | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/27/16

Nay wa Mitego adai ‘Free Nation 966’ itakuwa lebo tofauti na zingine

Rapper wa muziki kutoka Bongo, Nay wa Mitego amepanga kuachia wimbo wa kwanza kutoka kwa msanii wake chini ya lebo yake ya ‘Free Nation 966’.
13392718_216784082048425_2118719859_n
Lebo hiyo ya Nay wa Mitego inamiliki wasanii watatu lakini kwa kuanza amepanga kuachia wimbo wa msanii wake aitwaye ‘Tiki’.
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, kinachoruka kupitia EATV, Nay wa Mitego alisema lebo yake itakuwa na utofauti na lebo nyingine kutokana na yeye kuwa kuwa mfanyabiashara.
“Unajua mimi ni msanii wa kwanza kuanza kusimamia wasanii wenzangu, mpaka sasa nina wasanii watatu ambao wapo chini ya Free Nation, lakini kwa kuanza tutaanza na mmoja ambaye tushakamilisha naye kila kitu anaitwa Tiki,” alisema Nay.
“Nadhani Lebo yangu itakuwa na utofauti na Lebo nyingi sababu moja mimi ni mfanyabiashara hivyo hata msanii naye mleta lazima anaiingizie pesa huku akiwakonga mashabiki zake kwa muziki mzuri,” aliongeza.

google+

linkedin