6/24/16

Noti bandia Zasambaa Nchini, Wananchi Watahadharishwa

Meneja Msaidizi Kitengo cha Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Gloria Mwaikambo ametoa rai kwa wananchi kuwa makini na fedha bandia ili kuepuka hasara.


Mwaikambo amesema tatizo la noti bandia limekuwa kubwa nchini, kwani wananchi wengi hawajui jinsi ya kuzitambua.


Mwaikambo amesema hayo jana mjini Mbeya kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.


Amesema tatizo hilo limeenea nchi nzima, hivyo amewataka wananchi watambue alama 11 za kutambua fedha halali na bandia.


Wakati huo huo, Katibu Tawala Wilaya ya Kyela, Geofrey Anania ameishauri BoT kuhakikisha inaimarisha thamani ya shilingi ili kuleta ushindani kwenye Soko la Kimataifa, tofauti na sasa inaonekana kuzidiwa na fedha za kigeni.
 
Chanzo: Mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts