6/13/16

Picha: Kikao cha Bunge la Bajeti chaendelea leo Jumatatu Juni 13, 2016 Bungeni Mjini Dodoma.


    Wabunge wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baadya kumalizika kwa sala ya kuliombea Bunge leo asubuhi mjini Dodoma na  wakiendelea na msimamo wao  wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.


 Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) Mhe. Waitara Mwikwabe akiwa pamoja na Mbunge wa Same Mashariki (CHADEMA) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mary wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge hilo leo mjini Dodoma kuendeleas na msimamo wao wa wao  wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.


   Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto) na Lucy Magereli (katikati) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge hilo leo asubuhi mjini Dodoma.    Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku   mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini Dodoma.


    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na  Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akibadilishana mawazo na Mbunge wa Sengerema (CCM), Mhe. William Ngeleja na Mbunge wa Kibaha Vijijini (CCM), Mhe.  Hamoud Jumaa (CCM)  mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, ushirikiano wa afrika mashariki na Kikanda, Mhe. Susan Kolimba, akisalimiana na Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Anna Tibaijuka mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo leo mjini Dodoma.


 Wabunge wa CCM kutoka kushoto Sadifa Juma (Donge), Augustine Vuma (Kasulu Kusini) na Innocent Bilakwate (Kyerwa) wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo leo.

(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA)
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm