6/30/16

Picha za matukio Bungeni leo.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmbunge wa Nkasi Ali Kessy Bungeni Mjini Dodoma Mapema leo.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia Bunge Mapema leo mjini Dodoma wakati wa kuhitimisha mkutano wa Tatu wa Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akiteta jambo na Waziri wa Elimu Sayansi  Teknolojia na mafunzo ya Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako Bungeni Mjini Dodoma leo.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva na ujumbe wake uliotembelea Bunge ili kumkabidhi Naibu Spika Ripoti  ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa  ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akikabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Bungeni Mjini Dodoma leo mara baada ya Kuahirishwa kwa Bunge.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wakwanza kushoto)akiangalia moja ya vitabu vilivyopo kwenye maktaba ya Bunge wakati wa Ziara ya Mwennyekiti huyo na Ujumbe wake Bungeni Mjini Dodoma leo .

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahamud Hamid akiwa ndani ya maktaba ya Bunge wakati wa Ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (watatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ujumbe wake mara baada ya ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma leo.kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva na kulia Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahamud Hamid.
.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (katikati)akiongoza ujumbe wa tume hiyo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo wakati wa Ziara ya kutembelea Bunge na kuwasilisha ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
 (Picha zote na Frank Mvungi-Dodoma)
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts