Polisi Mwanza yakamata makokolo 25 | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/10/16

Polisi Mwanza yakamata makokolo 25Polisi mkoani hapa imekamata nyavu haramu 25 maarufu kwa jina la makokolo na timba 85 ambayo ni mitego ya kienyeji ya samaki katika kambi ya wavuvi iliyopo visiwa vya Maisome na Kasarazi wilayani Segerema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema leo kuwa zana hizo zilikamatwa wakati wa operesheni maalumu iliyofanyika katika visiwa hivyo Juni 8.

“Polisi walifanikiwa kukamata zana hizi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watu wanaohusika na uvuvi haramu, ndipo tulipovamia na kukamata zana hizo,” amesema.

google+

linkedin