6/12/16

Polisi wazuia kongamano la ACT, sababu yashindwa kuelewekaChama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) kimezuiliwa kufanya kongamano kililopanga kulifanya siku ya Jumapili, katika ukumbi wa Millenium Towers ili kufanya uchambuzi wa bajeti ya 2016/2017 ambazo mchambuzi mkuu alitakuwa ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Mh. Zitto Kabwe.

Taarifa ambayo imetolewa na Mwnyekiti wa ACT-Wazelendo, Anna Mghwira amesema kuwa walipokea taarifa kutoka kwa mmiliki wa Ukumbi waliopanga kufanya kongamano hilo kuwa Polisi wamemkataza kuwaruhusu kufanya kongamano katika ukumbi huo bila kupewa sababu na kuwa ni agizo kutoka viongozi wa juu wa Polisi.Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira akizungumza na waandishi wa habari, Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa ACT, Shaaban Mambo na Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa ACT, Yeremia Maganja.

Alisema kabla ya katazo hilo waliambiwa kuwa kuanzia asubuhi Polisi walikuwa wametanda katika eneo la Ukumbi huo ili kuzuia kongamano hilo ambalo lilikuwa na nia ya kuchambua bajeti ya serikali kwa mwaka wa 2016/2017 lakini pia kwa kiongozi wao, Mh. Zitto kupata nafasi ya kuelezea aliyopanga kuzungumza bungeni.

“Juhudi tunazozifanya hazitafanikiwa bila kuwa na demokrasia mwenye ukumbi katupa taarifa kuwa Polisi wamemkataza huku ni kunyimwa haki ya kidemokrasia tutakaa kama chama na kuangalia tunafanya nini,” alisema Mghwira.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa ACT, Yeremia Maganja alisema baada ya taarifa hizo kutoka kwa mmiliki wa ukumbi waliwasiliana na Kamishna Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro lakini na yeye aliwaeleza kuwa hana taarifa kuhusu kongamano hilo.Waandishi wa habari wakichukua habari kwa ajili ya kuuhabarisha umma.

“Polisi walimwambia mmiliki wa ukumbi kuwa akituruhusu angefungiwa biashara na ni agizo kutoka kwa Kamanda wa Kanda Maalum, baada ya kuwasiliana na Kamanda Sirro na yeye akasema kuwa hana taarifa sasa tunashindwa kufahamu kama wanashinikizwa na mamlaka fulani,” alisema Maganja.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts