Raia wa Nigeria afungwa maisha Tanzania | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/11/16

Raia wa Nigeria afungwa maisha Tanzania
Mfanyabiashara raia wa Nigeria, Joachim Ikechukwu Ike (36), amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha kilo 6,969.38 za dawa za kulevya aina ya Heroin.


Ike ambaye alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), Mei 11,2013, amehukumiwa adhabu hiyo jana na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Benedict Mingwa.


Jaji Mingwa amesema upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili mwandamizi wa Serikali, Tamari Mndeme, umeithibitishia mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.


Awali, Tamari akisaidiana na mawakili wenzake waandamizi,Saraji Iboru na Jullius Semali, alidai mshtakiwa alikuwa anataka kusafirisha dawa hizo zenye thamani ya Sh313.6 milioni kwenda Burkina Faso.

google+

linkedin