6/28/16

Saba saba Yaanza Leo, Nchi 30 na Kampuni 2500 Kushiriki

MAONESHO ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanaanza leo yakishirikisha nchi 30 na kampuni za ndani na nje ya nchi 2,500 zimethibitisha kushiriki.
Licha ya kuwapo kwa idadi hiyo iliyothibitisha kushiriki maonesho hayo yanayotarajiwa kufunguliwa rasmi Julai mosi mwaka huu na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, bado washiriki wengi hawajakamilisha maandalizi katika mabanda yao.Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Anna Bulondo alisema, hadi jana mchana kampuni 2,000 za ndani na 500 kutoka nchi 30 zimejiandikisha kushiriki na kupewa maeneo ya kuonesha bidhaa na huduma zao.
“Mwaka jana tulikuwa na kampuni 2,300 hivyo mwaka huu tuna ongezeko la asilimia nane huku kampuni za ndani zikiongezeka kwa asilimia 20, jambo ambalo limeakisi mwitikio mkubwa kwa maonesho yetu,” alisema Bulondo.
Bulondo alisema wizara saba na taasisi zake zinashiriki katika maonesho hayo ya mwaka huu na zinaendelea na maandalizi pamoja na taasisi nyingine za serikali zinazojitegemea kama Bunge na za wafanya biashara.
Alizitaja wizara hizo kuwa ni Wizara ya Fedha na Mipango; Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Maliasili na Utalii; Mambo ya Ndani ya Nchi; na Nishati na Aidha Bolondo alizitaja baadhi ya taasisi za wafanyabiashara kuwa ni Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Chama cha Wafanyabiashara Wanawake (TWCC), Pride, Mfuko wa Fursasawa kwa Wote (EOTF), Shirika la Viwanda Vidogo (Sido) na Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania.
Nchi shiriki ni Afrika Kusini, Australia, Bulgaria, Brazil, China, Ghana, Ufaransa, India, Indonesia, Italia, Iran, Japan, Kenya, Korea Kusini, Malawi, Mauritius, Misri, Msumbiji, Pakistan, Singapore, Syria, Uganda, Uingereza, Ujerumani, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bulgaria, Rwanda, Sudani Kusini na Vietnam.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm