6/8/16

Serikali na Wadau wa Maendeleo kutumia Dola Bilioni 3.3 kutekeleza programu ya sekta ya maji
Ismail Ngayonga- Dodoma
SERIKALI kwa kushirikiana  na wadau wa maendeleo imepanga kutumia kiasi cha Dola Bilioni 3.3 ili kutekeleza awamu ya pili ya programu ya maendeleo ya sekta ya maji nchini 2016/17 hadi 2020/21.
Akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa Buhingwe (CCM), Albert Obama, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe, alisema awamu ya pili ya programu hiyo tayari imeanza mwezi Januari mwaka 2016.
Kamwelwe alisema Wizara yake itahakikisha kuwa inaajiri wataalamu wa kutosha ili kila Halmashauri iweze kutelekeleza programu hiyo kwa mafanikipo makubwa zaidi.
“Pale ambapo halmashauri yeyote itakuwa na tatizo la ukosefu wa watumishi, Wizara yangu itatuma wataalamu wake katika halmashauri hiyo ili kuhakikisha kuwa wananchi wetu wananufaika na programu hiyo” alisema Kamwelwe.
Mbunge huyo wa Buhingwe alitaka kufahamu ni lini programu ya mradi wa maji katika jimbo la Buhingwe utaanza kutekelezwa.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge huyo, Kamwelwe alisema kutokana na ahadi aliyoitoa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Serikali ilituma pesa katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kiasi cha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya kufanya usanifu wa mradi.
Aidha aliongeza kuwa kutokana na andiko la ukarabati wa mradi huo kugharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 1, Serikali ilipanga kuutekeleza mradi huo katika awamu ya pili ya programu ya maendeleo ya sekta ya maji.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts