6/1/16

Silinde Agoma Kusoma Hotuba ya uUpinzani

 Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Wizara
Msemaji wa Kambi ya upinzani kwa Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde amegoma kusoma hotuba ya kambi hiyo bungeni kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa Naibu Spika, Tulia Ackson katika kuliendesha Bunge.
Baada ya Kamati ya Bunge ya Bajeti kuwasilishwa taarifa yake, Dk Tulia alimtaka msemaji wa upinzani kuwasilisha taarifa yake, bila wabunge wengine wa upinzani kuwamo ndani ya Bunge kumpinga naibu spika.
Baada ya kuitwa, Silinde alitokea nje moja kwa moja na kusema kuwa anaomba hotuba ya Kambi hiyo iingie kwenye kumbukumbu za Bunge kama ilivyo ila hataisoma kutokana na kutoridhishwa na Naibu Spika, kisha akatoka nje.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm