6/12/16

Simu feki zawashwa, zazima kupima ukweli


MAMLAKA ya Mawasiliano (TCRA), imesema wananchi wamekuwa wakizizima na kuziwasha mara kwa mara simu feki zilizo katika mitandao ya mawasiliano nchini, ingawa matumizi yake kwa ujumla yamepungua.

Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi alisema katika mazungumzo na Nipashe, jijini Dar es Salaam juzi kuwa wananchi wamekuwa wakiziwasha simu feki na kuzijaribu mara kwa mara ili kufahama kama zimeshazimwa tayari ama la.

Mungi alikuwa akizungumza na Nipashe kuhusu uzimawaji wa simu hizo ifikapo Alhamisi.

“Takwimu zetu zinaonyesha simu feki zimepungua sana, wananchi wameelimika, maeneo mengine unakuta kati ya watu 200 wanaotumia siku hakuna simu feki au ipo moja,” alisema Mungi.

Alisema changamoto kubwa iliyobaki ni wananchi kutoamiani kama kweli zitazimwa.

Alisema hali hiyo inawafanya watu wenye simu feki ambao walishaacha kuzitumia, waziwashe simu zao kwa muda na kuzizima.

Lakini “mpango wetu uko pale pale," alisema Mungi. "Simu feki lazima zizimwe Juni 16 mwaka huu, na tunaandaa taarifa ya kina juu ya tukio hili.”
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts