6/19/16

TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

 
Tarehe 16-23 Juni kwa kila mwaka ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo Sekretarieti ya Ajira kama Taasisi nyingine Serikalini hukutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu na ufafanuzi juu ya utekelezaji wa majukumu yao. Kwa upande wa Sekretarieti ya Ajira tumekuwa tukipokea maswali/maoni/hoja mbalimbali zinazohusu mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma kutoka kwa wadau mbalimbali.

Katika maadhimisho hayo kwa mwaka huu 2016 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametenga siku maalum ya tarehe 21 Juni, 2016 kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni kwa ajili ya kupokea maoni, hoja na maswali mbalimbali yanayohusu mchakato wa Ajira Serikalini ambapo wadau wetu wanaweza kupiga simu katika namba zifuatazo na kuongea na Viongozi wa Sekretarieti ya Ajira moja kwa moja na wataweza kuuliza maswali na kupatiwa majibu kupitia 0762-752968, 0784-398259 au 0687-624975, pia kwa kuandika hoja, maswali ama malalamiko kwenye anuani zifuatazo;- malalamiko@ajira.go.tz, gcu@ajira.co.tz, facebook.com/psrsajira na twitter.com/psrsajira ambapo yatajibiwa papo hapo.

Aidha, kwa wale ambao wanaona maswali au maoni yao lazima wayafikishe wenyewe kwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira basi wanakaribishwa siku ya tarehe 21 Juni, 2016 ambapo Katibu ametenga ili kukutana na wadau mbalimbali.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, 16 Juni, 2016.2
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts