‘Tanzania ina wataalamu wachache wa kutoa dawa’ | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/22/16

‘Tanzania ina wataalamu wachache wa kutoa dawa’

TANZANIA ina wataalamu wachache wenye taaluma ya kutoa dawa katika zahanati na vituo vya afya hasa vijijini, huku Serikali ikitakiwa kuangalia suala hilo ili kuboresha huduma na usalama wa afya za wananchi.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St John, Profesa Emmanuel Mbena alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya mwaka moja ya ngazi ya Cheti kwa watoa huduma ya dawa.
Alisema kozi hiyo inatolewa kwa kushirikiana na Serikali ya Sweden chini ya Mradi wa Kukuza na Kuimarisha Mfumo wa Afya (HPSS).
Alibainisha kuwa ni vyema Serikali ikaunga mkono katika kufadhili wanafunzi. Kwa upande wake, aliyekuwa Msajili wa Baraza la Wafamasia, Moldred Kinyawa alisema harakati za kuanzisha kozi hiyo zilianza tangu mwaka 2007, ambapo mwanzoni waliomba kozi hiyo pia itolewe na taasisi binafsi.
Naye, Dk Karin Wiedenmaryer kutoka HPSS, alisema watoa dawa wanahitaji mafunzo ili wapate kutoa huduma inavyostahili. Mmoja wa walimu wa kozi hiyo, William Kidenya alisema kuna matatizo mengi yanatokea hasa vijijini ambapo watoa dawa wengi katika vituo vya kutolea huduma hawana taaluma hiyo.
Alisema wengi wanatoa dawa bila kujali vipindi wala aina yake, hali ambayo imekuwa ikichangia matatizo kama ya magonjwa wa figo.
Mratibu wa HPSS, Fiona Chilunda alisema HPSS watafadhili mafunzo hayo kwa miaka miwili, ambapo gharama za mradi huo hadi kufikia Julai 30, mwaka huu zitakuwa Sh milioni 139 na mwaka utakaofuata gharama hizo zitapungua na kufikia Sh milioni 100.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, James Charles alisema asilimia 96 ya watoa huduma ya dawa katika mkoa wa Dodoma hawana ujuzi.

google+

linkedin