6/21/16

Tanzania na Uganda zatakiwa kusitisha uwindaji

Serikali ya Tanzania na Uganda, zimeshauriwa kusitisha kwa muda uwindaji wa kitalii wa tembo ili kudhibiti matukio ya ujangili ambayo yanaendelea kupunguza idadi ya wanyama hao duniani.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Elephant Neighbors Center ya Kenya, Jim Nyamu ametoa wito huo wakati akiongoza matembezi ya kilomita 3,200 katika nchi za Afrika ya Mashariki kupinga mauaji ya tembo ambayo yamefika Arusha.


Matembezi hayo yameanzia Nairobi Kenya kwa kuzinduliwa na Mke wa Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta, Margaret na yanatarajiwa kufika jijini Dar es Salaam Julai 6 na kupokewa na Mke wa Rais John Magufuli, Janeth na baadaye kuendelea nchini Uganda.
 
chanzo: Mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts