6/12/16

Tetesi za Soka Ulaya, ziko hapa
Tunakuletea tetesi zaz soka la Ulaya leo hii.
Uhamisho wa Zlatan Ibrahimovic kwenda Manchester United umesimama kwa muda wa kuwa mchezaji huyo anataka kucheza katika michuano ya Olimpiki ya mwezi Agosti (Sunday Mirror), Arsenal wataanza kumfuatilia Edinson Cavani, 29, iwapo Jamie Vardy, 29, atakataa kwenda Emirates. Cavani anataka kuondoka PSG na amekataa mkataba mnono wa kwenda China (Sunday Express), Arsenal pia wanafikiria kupanda dau la pauni milioni 15 kumtaka beki wa kimataifa kutoka Albania Elseid Hysaj, 22, anayechezea Napoli (Daily Star Sunday), Real Madrid wataambiwa na Juventus kuwa kumpata Paul Pogba, itawagharimu pauni milioni 94.7 pamoja na kiungo Toni Kroos (Marca), kipa wa Manchester United ana hadi Jumatano kuamua iwapo ajiunge na Real Madrid kwa pauni milioni 47, kabla ya kifungu maalum kwenye mkataba wake hakijaisha muda wake (Sunday Times), Manchester City wameambiwa lazima wavunje rekodi ya Uingereza na kulipa pauni milioni 65 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, 26 (Sunday Mirror), N'Golo Kante, 25, amepewa mkataba wenye mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki na Leicester City. Kiungo huyo kutoka Ufaransa anasakwa na Chelsea, Manchester United, Arsenal na Paris St-Germain (Sunday Telegraph), Juventus wamejiunga kwenye mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku, 23 (Gazeetta Dello Sport), kiungo wa Roma Miralem Pjanic, 26, aliyehusishwa na kuhamia England, atafayiwa vipimo vya afya Juventus (Guardian), Burnley waliopanda daraja EPL wanamtaka kipa wa West Brom Boaz Myhill, 33 (Birmingham Mail), Liverpool wanapanga kumtumia Jordon Ibe, 20, kama chambo kumsajili Sadio Mane, 24, kutoka Southampton kwa pauni milioni 30 (The Sun). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Siku njema

Imeandaliwa na Salim Kikeke
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts