6/20/16

Tetesi za usajili zilizoshika Juni 20,2016


Habari kubwa kwa sasa barani Ulaya zinahusu uhamisho wa wachezaji kutoka klabu moja kwenda nyingine wakati timu zikinuwia kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa mwaka 2016/17.Mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Napoli ya Italia Gonzalo Higuain (pichani) anayetajwa sana katika dirisha hili la majira ya kiangazi ya usajili.


Zifuatazi ni tetesi kubwa za usajili ambazo zimechukua nafasi kubwa:-

1-Gonzalo Higuain kutoka Napoli kwenda Atletico Madrid
Mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya Taifa ya Argentina Gonzalo Higuain anatajwa kutaka kuhamia katika klabu ya Atletico Madrid ya Hispani.

Hata hivyo mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid amesema kwa sasa atahitaji utulivu mpaka kumalizika kwa michuano ya Copa America inayorindima huko Marekani.

2-Pierre Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester City.

Licha ya kuwa kocha wa Klabu ya Manchester City Pep Guardiola kuhitaji huduma ya mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang, klabu hiyo haipo tayari kulipa kitita cha pauni milioni 65 kwa klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Wakati huohuo klabu hiyo imetenga dau la pauni milioni 16.7 kwa ajili ya kumnyakua mshambuliaji wa Las Palmas ya Hispania Mbrazil Gabrieli Jesus ambaye pia anawaniwa na klabu za Manchester United na Bayern Munich.

3-Emanuele Giaccherini kutoka Sunderland kwenda Chelsea

Mshambuliaji Emanuele Giaccherini anayetikisa vilivyo na timu yake ya Taifa ya Italia amesema anataka kuungana na kocha Antonio Conte katika maisha yake mapya na klabu yake ya Chelsea.

5-Ramiro Funes Moro kutoka Everton kwenda Barcelona

Mabingwa wa La liga Fc Barcelona wanamfuatilia kwa karibu nyota wa Everton ya Uingereza Ramiro Funes Mori aliyeonekana kufanya vyema katika ligi kuu msimu uliopita.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts