6/22/16

TFDA yakamata tende mpakani zinazodaiwa kuingizwa nchini kinyemela

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imekamata tani laki sita za tende mpakani mwa Kenya na Tanzania eneo la Hororo zilipokuwa zikiingizwa nchini kwa ajili ya kuanza kuuzwa.

Mkurugenzi wa TFDA, Thomas Nkoro amesema: “Tumezikamata tende hizi kwakuwa hazina taarifa ya aina yoyote kwa mlaji na zilikuwa zimefungashwa katika vifungashio visivyo faa.”


Amesema zilikuwa zimehifadhiwa kwenye magunia na madumu ya bati ambayo si rafiki kwa afya ya binadamu.

Hata hivyo, amesema Tende hizo zinasadikika kuwa tayri zilishapata kutu kutokana na vifungashio vyake na tayari baadhi ya watu waliokula tende hizo wameanza kulalamika kuumwa tumbo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts