6/2/16

Ulaya yataka Tanzania iruhusu mgombea binafsi

Mwangalizi Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa

Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU-EOM), umewasilisha ripoti yake kamili yenye mapendekezo ya marekebisho ya kuboresha mchakato wa uchaguzi, ikiwamo la kutaka Tanzania iruhusu mgombea binafsi wa urais.


Mwangalizi Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa EU, Judith Sargentini amesema licha ya uchaguzi wa Oktoba 25, 2015 kuonyesha dhamira ya Watanzania ya kuzingatia mfumo wa kikatiba na kuheshimu misingi ya demokrasia, kulikuwa na kasoro kadhaa.


Amesema taasisi za usimamizi wa uchaguzi, hazikuonyesha uwazi kamili juu ya michakato yao ya kufanya uamuzi.


Kuhusu Zanzibar, amesema licha ya tamko lao la awali kuelezea wasiwasi wao mkubwa na kuiomba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) iwasilishe ushahidi wa kuhalalisha uamuzi wa kufuta matokeo, hadi sasa haijafanya hivyo.


Katika mapendekezo yao, wameshauri kuruhusiwa kwa haki ya kugombea kama mgombea binafsi kwa ajili ya uchaguzi wowote wa Muungano au Zanzibar; haki ya kulalamikia matokeo ya uchaguzi wa rais katika sheria na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015 itumike kwa uwiano, ili kulinda haki ya kujieleza na haki ya kuwa na kesi isiyo na upendeleo.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm