6/19/16

UN waandaa mkutano wa albino leo
Umoja wa Mataifa (UN) umeandaa mkutano mkuu wa kwanza wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) Afrika unaolenga kutathmini mauaji ya watu wenye hali hiyo.


Mtaalamu wa Masuala Huru ya Ualbino kutoka UN, Ikponwosa Ero amesema mkutano huo unaoanza leo nchini utahudhuriwa na nchi 28 na watu zaidi ya 150, umelenga kutoa suluhu au njia zinazotekelezeka katika kukabiliana na mauaji ya albino.


“Kwa Tanzania kiini kikuu cha mauaji haya ni ushirikina, Serikali ina wajibu wa kuwatofautisha na kuwapa usajili wale wanaotibu kwa tiba asili ili kuwabana waganga wa kienyeji wanaohusika zaidi na mauaji ya watu wenye ualbino,” amesema.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm