6/21/16

Vigezo ugawaji fedha za umma kupitiwa upyaWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Serikali inapitia upya vigezo vya ugawaji wa fedha za ununuzi wa dawa ili kuepuka vituo vyenye watu wengi kugawiwa fedha zisizoendana na idadi ya wananchi wa eneo husika.

Amesema hayo jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood aliyetaka kujua Serikali inachukua hatua gani katika kuwezesha upatikanaji wa mashine za X-ray katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Akijibu swali hilo, Mwalimu amesema hivi sasa hakuna mgawanyo wa uwazi wa fedha za ununnuzi wa dawa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma nchini.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts