6/19/16

Waandamana kupinga uwepo wa jeshi la Marekani Okinawa

 
Maelfu ya watu wamejumuika pamoja katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan, katika mojawepo ya maandamano makubwa katika kipindi cha miongo miwili, kupinga uwepo wa wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo.
Waandamanaji wana hasira kuhusiana na madai ya ubakaji na mauwaji ya kijana mmoja mwanamke wa eneo hilo, yaliyotekelezwa na mwanajeshi wa zamani wa majini wa Marekani, wanaoishi katika kisiwa hicho.
Kisa hicho kimefufua upinzani mkubwa kisiwani Okinawa dhidi ya kambi ya wanajeshi wa Marekani kisiwani humo.
Mipango ya kuondoa kambi hiyo haijafua dafu.

BBC
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts