6/11/16

Wachezaji 6 wa Azam FC wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa klabu


Baada ya mashabiki wa klabu ya Azam FC kupewa nafasi ya kupiga kura kuwachagua wachezaji bora wa klabu, leo June 11 2016 Azam FC kupitia tovuti yake ilitaja majina ya wachezaji sita wa Azam FC waliofanikiwa kuignia fainali ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa klabu hiyo.
Jumla ya kura 810 zilipigwa kuchagua wachezaji bora wa klabu hiyo, kura 200 ziliharibika. Shomari Kapombe aliongoza kwa kupata kura 277, Aishi Manula kura 120, Pascal Wawa kura 40, Himid Mao kura 30, Farid Mussa na Ramadhani Singano ‘Messi’ wamelingana kura kwa kupata kila mmoja 27.
Zoezi la upigaji kura kumtafuta mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo linaendelea le Jumamosi ya June 11 hadi Jumatano ya June 15 na saa 6 mchana mshindi atatangazwa rasmi.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts