Wanafunzi mnaouza miili acheni tabia hiyo- Samia | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/18/16

Wanafunzi mnaouza miili acheni tabia hiyo- Samia

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MMama Samia Suluhu amewataka baadhi ya wanafunzi wa vyuo nchini kuacha tabia ya kuuza miili yao kwani tabia hiyo inadhalilisha wazazi jamii na hawa wanafunzi hao na masomo wanayosoma.

Makamu wa Rais ameyasema hayo alipokuwa akihutubia siku ya wahitimu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe ambapo lengo lilikuwa ni kufanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana wanaosoma chuoni .

Makamu wa Rais katika hotuba yake akatumia nafasi hiyo kuwaasa wanafunzi wa kike wanaosoma chuoni hapo kuacha tabia ya kuuza miili yao huku akitaja hoteli na maeneo ambayo wanafunzi hao wamekuwa wakijichanganya.

‘’Leo wanafunzi wa vyuo wanaongoza kwa kuuza miili yao jambo ambalo linasikitisha sana tabia hii ni mbaya acheni mara moja’’- Amesema makamu wa Rais Mama Samia.

Aidha Makamu wa Rais amesisitiza kuwa wataalamu wa sekta ya elimu nchini wana wajibu wa kutizama upya mitaala ya elimu inayotolewa vyuoni ili iweze kuendana na soko la ajira pamoja na ujuzi wa kujitegemea.

Katika harambee ya kuchangia bweni hilo jumla ya shilingi milioni 262.4 zimepatikana ikiwa ni jumla na ahadi ambapo wageni mbalimbali wameahidi kuendelea kuchangia chuo hicho huku makamu wa Rais akiahidi kuchangia milioni moja kutoka katika mshahara wake wa kila mwezi kuanzia mwezi wa saba

google+

linkedin