6/26/16

Wanafunzi wateketeza mabweni 10 magharibi mwa KenyaMasomo katika shule ya upili ya Itierio iliyo Kisii Magharibi mwa Kenya, yamesitishwa baada ya wanafunzi kuchoma jumla ya mabweni kumi kupinga sheria mpya zilitongazwa na usimamizi wa shule.

Kisa hicho pia kilisababisha mali ya thamani kubwa kuharibiwa. Wanafunzi pia walivamia ofisi ya mwalimu muu, duka la shule na mahabara ya shule jirani ambapo walifanya uhiribifu.

Ghasia zilianza Jumamosi usiku wakati wanafunzi walinyimwa fursa ya kutizama mechi za kombe la taifa bingwa barani Ulaya ambapo wanafunzi walidai kuwa hiyo ni moja ya sheria ngumu zilizowekwa shuleni humo.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm