6/18/16

Watanzania wana hatari ya kupata kiharusi kuliko Waingereza

 Mwenyekiti wa Muungano wa Magonjwa
Utafiti wa Steps umeonyesha kuwa Watanzania wana hatari mara sita zaidi ya raia wa Uingereza kupata ugonjwa wa  kiharusi.
Magonjwa mengine ni kisukari, saratani na unene kupita kiwango.
Mwenyekiti wa Muungano wa Magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA), Dk Tatizo Waane amesema jana kuwa utafiti huo ulilenga kuangalia ukubwa wa tatizo la magonjwa yasiyoambukiza.
Akielezea athari za magonjwa yasiyoambukiza duniani, Makamu Mwenyekiti wa TANCDA, Profesa Andrew Swai amesema zaidi ya vifo milioni 56 vinavyotokea kila mwaka husababishwa na magonjwa hayo ikilinganishwa na vifo milioni 38 vitokanavyo na magonjwa ya kuambukiza.
Dk Swai amesema nchini kuna mengi yanayotakiwa kufanyika kupunguza magonjwa yasiyoambukiza na athari zake.

Chanzo: Mwananchi
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm