6/18/16

Watoto 100 kupata akaunti CRDB
Zaidi ya watoto 100 wilayani Kibaha mkoani Pwani wanatarajia kuingizwa kwenye akaunti ya watoto kupitia Benki ya CRDB Tawi la Kibaha, lengo likiwa ni kuwawezesha kuwa na uhakika wa kumudu gharama za masomo kwa kipindi cha baadaye.
Hayo yalibainishwa jana na Meneja wa CRDB wa tawi hilo, Rosemary Nchimbi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika na kuwa, benki hiyo imeamua kutumia maadhimisho hayo kuweka punguzo la gharama ya kufungulia akaunti kutoka Sh20,000 hadi 10,000 kwa mtoto mmoja.
"Tumeona ni jambo la busara kutumia maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kutoa punguzo la gharama za kufungua akaunti ya mtoto kutoka kiasi cha Sh20,000 hadi sh.10,000 kwa mtoto mmoja na hii akaunti lengo lake ni kumsaidia kuwekewa akiba ya pesa na mzazi au mlezi wake ana pesa hizozitamsaidia gharama zamasomo kwa kipindi cha baadaye, "alisema.
Baadhi ya wazazi waliofika kuwafungulia watoto wao akaunti hiyo, Godfrey Munishi na Janeth Makungu waliishukuru CRDB kutumia maadhimisho hayo kutoa punguzo la gharama za kufungua akaunti ya mtoto na kuomba benki zingine kuiga mfano huo
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm