6/25/16

Wavuvi Kojani waokota bawa la ndege kubwa

 
Wavuvi wa Kisiwa Kidogo cha Kojani Wilaya ya Wete, Pemba, wameokota kipande cha bawa linalodhaniwa ni mabaki ya ndege ya Malyasia iliyopotea Machi 8, mwaka 2014.
Bawa hilo lenye urefu wa futi nane na inchi moja, limeokotwa majini katika mapango eneo la Ng’ombe nyuma ya Kisiwa cha Kojani.
Wavuvi waliookota bawa hilo, Chungua Hamad Chungua, Juma Mbwana Kombo, Mbwana Bakar Mhunzi, Hamad Chungua Faki na Bakar Hamad Chungua walisema lilikuwa ndani ya mapango na wanahisi huenda lilikuwapo muda mrefu kwani limeanza kuota kutu.
“Tulipoliona tulitoa taarifa  serikalini, tulikuwa hatufahamu ni bawa la kitu gani, lakini baada ya muda tukaambiwa ni la ndege,” alieleza mmoja wa wavuvi hao.
Katibu Tawala Wilaya Ndogo ya Kojani, Makame Khamis Makame amesema tayari wataalamu kutoka ofisi ya meneja wa usafiri wa Unguja, Pemba wamefika kuchukua vipimo na maofisa kutoka Makao Makuu ya Mamlaka ya Anga, Dar es Salaam wameshafanya uchunguzi wa kitaalamu.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm