Waziri mkuu wa India Narendra Modi ahotubia bunge la Marekani | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/9/16

Waziri mkuu wa India Narendra Modi ahotubia bunge la Marekani

Waziri mkuu wa India Narendra Modi akihotubia bunge la Marekani

Kama kiongozi wa taifa liillokumbwana na migawanyiko ya madhehebu, kidini na kikabila, waziri mkuu wa India Narendra Modi anatafuta uwelewano na wabunge wa marekani kwa kutumia ucheshi.

Bw Modi aliwaambia wabunge wa Marekani kuwa nimeambiwa kazi ndani ya bunnge zinafanyika kwa Amani. Anasema pia nimeambiwa kuwa mnajulikana sana kwa ushirikiano baina ya vyama vyenu. Bw Modi alipigiwa makofi vikifuatiwa na vicheko baada ya kutoa kauli hiyo, pale alipokutana na wabunge wa Marekani hapo jana.

Bw Modi aliendelea kuwaambia wabunge hao kuwa hawako peke yao. Alisema, mara kwa mara yeye pia hushuhudia hali kama hiyo katika bunge la India. Kwa hivyo tuna mifano mingi ya pamoja.

Bw Modi alisema kushamiri kwa ushirikiano wa biashara na nishati, na hata maslahi ya kimkakati, na kuongezea kuwa umbali na hali ya kutokuaminiana amabyo awali iliashiria uhusiano wa India na Marekani, sasa ni jambo la zamani.

Anasema uhusiano wetu umevuka kusitasita za historia, na sasa ukweli na muunganiko unafafanua majadiliano yetu, na bw Modi alisihi kuwepo na ushirikiano wa karibu zaidi kwa malengo yao pamoja.

Hotuba ya Modi ilikuwa ni ya tano kuwahi kutolewa na mkuu wa serikali ya India kwa bunge la marekani. Hotuba hio inafwatia mkutano wa jumanne na rais Barack Obama na tangazo kuwa India itajenga vinu 6 vya nuklia vitakavyojengwa na makampuni ya marekani, hiyo ikiwa matokeo ya makubaliano ya kiraia ya kinuklia kati ya mataifa hayo mawili ambayo yalifikiwa mwaka 2008.

google+

linkedin