6/24/16

Wema Atoboa Siri Yake na Zari


WEMA2Wema Sepetu.
Stori: Imelda Mtema, Ijumaa
Dar es Salaam: Kwa mara ya kwanza, staa kiwango kunako sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ametoboa siri iliyofichika anayoijua mwenyewe kati yake na mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akieleza kuwa, hajawahi kumchukia wala kufikiria kumchukulia bwana’ke ila baadhi ya wapambe wake wamekuwa wakichochea kuwepo kwa bifu kati yao.
zariZari.
KISIKIE CHANZO
Mmoja wa watu wa karibu wa mlimbwende huyo wa Tanzania mwaka 2006/07 aliyeomba jina lisichorwe gazetini aliling’ata sikio Ijumaa kuwa, Wema amekuwa akiumizwa na madai kuwa anamchukia Zari ‘Mama Tiffah’ wakati katika uhalisia siyo hivyo.
“Wema amekuwa mgumu sana kumzungumzia Zari lakini safari hii ni kama uzalendo umemshinda kutokana na maneno ya watu hasa hili la kumzushia kuwa karudiana na Diamond.
“Mwenyewe anasema hana tatizo na Zari ila hizi Timu Zari, Timu Diamond na Timu Wema ndizo zinachochea mambo, hata kama ni madogo yanakuzwa,” kilidai chanzo hicho.
Wema na Diamond
diamond-na-wema
IJUMAA LAMSAKA WEMA
Katika kutaka kupata maneno hayo kutoka kwa Wema mwenyewe, hivi karibuni mwandishi wetu alimpigia simu na kumuuliza kilichopo kati yake na Zari kwani yamekuwa yakisemwa mengi likiwemo hili la kwamba sasa hivi bifu limekolea baada ya Wema kudaiwa kumrudia Chibu (Diamond).
Alipopatikana Wema alifunguka: “Ninachotaka kusema leo ni kwamba, Zari anatakiwa kuwa na amani na familia yake, wala asisikilize maneno ya watu kwa sababu mimi siwezi kumuingilia kwenye uhusiano wake.
“Kwa Chibu ilikuwa zamani lakini kwa sasa yeye ana maisha yake na mimi nina maisha yangu. Sasa kama Zari atakuwa anaendelea kuwasikiliza watu wa pembeni, hilo litakuwa ni tatizo lake.
“Kitu ambacho wengi hawakijui ni kwamba mimi sijawahi kumchukia wala kuwaza kumfanyia ubaya Zari. Pia sina mpango wa kumchukulia bwana’ke (Diamond) kwa kuwa sina sababu ya kufanya hivyo.”
zari-diamond4Zari na Diamond
ATAMANI KUKUTANA NAYE
Katika kuonesha kuwa, analo la ziada linalomkereketa moyoni la kumwambia bishosti huyo, Wema alisema kuwa anatamani siku moja akutane naye ana kwa ana ili wazungumze.
“Kwa haya yote yanayotokea, kiukweli natamani sana kukutanishwa naye, nikikutana naye nimwambie kilicho moyoni mwangu, nimpe ukweli wake kwamba hizi timutimu zinamuingiza ‘choo cha kike’, akiwasikiliza hao wapambe watakuwa wakimpoteza na kumpa uzushi unaoweza kumkosesha amani wakati hana sababu ya kuwa hivyo,” alisema Wema.
ZARI ANASEMEJE?
Kwa muda mrefu kumekuwa na ugumu wa kumpata Zari kuzungumzia uhusiano wake na Wema na sababu za figisu zao, ila hivi karibuni mpenzi huyo wa sasa wa Diamond alimzungumzia Wema ambapo alisema yeye kama mzazi anaposikia Timu Wema wanasema Tiffah (mtoto wa Diamond) ni mtoto wa Katunzi (pedeshee Mzamir Katunzi) au Ivan (aliyekuwa mume wa Zari) hawezi kukaa kimya.
“Kama ni mtoto wa Ivan au Diamond, yeye (Wema) na timu yake wanapunguza nini au wanaongeza nini? Diamond kawapitia Jokate ?(Mwegelo), (Jacqueline) Wolper lakini wametulia kwa nini yeye (Wema)?
“Kwa muda mrefu nilikaa kimya sana lakini hivi karibuni Timu Wema wameposti kusema mwanangu ni mbaya, eti ni zombi, kama mzazi nisingeweza kukaa kimya,” alisema Zari.
Maelezo yake hayo yanaonesha kuwa, ni kweli Zari amekuwa akifuatilia mambo ya Timu Wema mtandaoni akidhani wanaoandika vibaya kuhusu yeye na mwanaye wanatumwa na Wema, jambo ambalo linaweza kuwa halina ukweli.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts