6/25/16

Wema Sepetu: Nikiwajibu mtandaoni nawapa kikiMREMBO tishio kwenye kiwanda cha filamu za Tanzania, Wema Sepetu, ametoboa siri ya kutokujibu komenti za watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii hata kama wamemtusi au kumdhalilisha Wema Sepetu, ameliambia Papaso la Burudani kuwa anatambua thamani yake kama mtu maarufu hivyo anapowajibu watu wanaomtukana kwenye mitandao ya kijamii anakuwa anawapa umaarufu kitu ambacho hawastahili.

“Huwa nawajibu mara chache mno. Nafanya hivyo kwa sababu wengi wao wanafanya makusudi kunitukana ili wasikie Wema atajibu nini. Mimi najielewa ukubwa wa jina langu unaweza kumfanya mtu niliyemjibu kuwa maarufu ingawa sikustahili kumpa umaarufu huo,” alisema Wema.

Wema Sepetu, hivi karibuni amewashangaza mashabiki wake mara baada ya yeye na mpenzi wake wa zamani, Luis Mnana, kuanikana kwenye mitandao ya kijamii huku wakiandika maneno yaliyobeba hisia za kimapenzi kati yao.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm