6/25/16

Yanga Kutua Usiku wa Manane
KIKOSI cha Yanga kinatarajiwa kutua Dar es Salaam usiku kikitokea mjini Antalya, Uturuki, tayari kwa maandalizi yake ya mwisho kuelekea mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amelipasha BINGWA akisema: “Tunatarajia kuondoka huku Antalya kesho (leo) mchana kuja huko Tanzania na tutafika usiku.”

Saleh alisema maandalizi yote kwa upande wa wachezaji yamekamilika na wana matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo wa Jumanne ya wiki ijayo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Tunashukuru programu ya kocha imeenda kama ilivyopangwa na sasa tunarejea nyumbani kuja kufanya maandalizi yetu ya mwisho,” alisema.

Alisema wachezaji wote wa kikosi hicho wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo, ukiacha Amissi Tambwe na Haji Mwinyi ambao wataukosa kutokana na kutumikia adhabu zao za kadi.

Alisema mabeki; Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Said Juma Makapu ambao walikuwa wagonjwa, wameanza mazoezi ya nguvu na wenzao na kwamba kocha Hans van der Pluijm, ana uhakika mkubwa wa kuwatumia.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts