6/10/16

Yanga tayari kukabiliana na kila hali huko Algeria

Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga Juma Mwambusi amesema, wanaendelea kuwajenga wachezaji kisaikolojia ili kuweza kupambana katika mchezo ulio mbele yao dhidi Mo Bejaia.Mwambusi amesema, wanauangalia mchezo huo kwa jicho la tatu kwani wanajua mchezo utakuwa mgumu kwani wanakutana na timu ambayo ni nzuri pia, lakini anaamini mechi za awali walizocheza pamoja na mazoezi zitawasaidia kuweza kupambana kwa kujua wanakutana na timu gani na wanatakiwa kupambana kiasi gani.

Mwambusi amesema, mechi wanayoenda kucheza itakuwa na ushindani na hawajawahi kucheza na Waargeria hivi karibuni lakini wachezaji wanajua wanaenda kukutana na nchi za kiarabu na watakutana na mambo mengi lakini kikubwa ni maandalizi.

Mwambusi amesema, wanajua nini maana ya kucheza ugenini na maana ya kucheza nyumbani hivyo watakuwa na uwezo wa kupambana na fitna ambazo zitatengenezwa na wapinzani wao.
Mwambusi amesema, katika mchezo huo kila silaha zinatakiwa kufanya kazi ikiwa ni pamoja na mbinu za uwanjani pamoja na tahadhari ya kucheza Uwanja wa ugenini.

Mwambusi amesema, mpaka sasa wachezaji asilimia kubwa wameshawasili kwa ajili ya mazoezi isipokuwa beki wa kati wa Vincent Bossou ambaye ataungana na kikosi hivi karibuni.

Yanga itaanzia ugenini dhidi ya MO Bejaia ya Algeria June 17 mwaka huu katika mchezo huo wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts