7/19/16

Ajali yaua wawili, yajeruhi 18 GeitaKamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga.


Watu wawili wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.


Ajali hiyo ilitokea jana baada ya gari la abiria likitokea mjini Geita kwenda Senga kuacha njia na kupinduka.


Mkuu wa trafiki mkoani Geita, Alfredy Hussein alisema dereva wa gari hilo alitoroka baada ya ajali na uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali ni mwendo kasi.


Daktari wa kitengo cha dharura katika hospitali teule ya mkoani hapa, Mahenga Makoye alisema majira ya saa saba mchana walipokea majeruhi 19 baadhi yao wakiwa na hali mbaya.


“Tumepokea majeruhi 19 lakini wakati tukiwahudumia, mmoja wao aliyekuwa na majeraha makubwa sehemu ya kichwa alifariki, bado wengine wawili hali zao ni mbaya,” alisema Dk Makoye.


Dk Makoye alisema aliyefariki akipatiwa huduma ni mwanamke anayekadiriwa kuwa na miaka 25-27 na aliyefariki katika eneo la ajali ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri huo huo na majeruhi wengi wamevunjika viungo ikiwamo mikono na miguu.Alisema majeruhi wengine hali zao ni mbaya na wanafanyiwa utaratibu wa kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm