7/2/16

Alichojifunza JPM kwa Kagame
Katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi ambayo alikwenda Rwanda, Rais John Magufuli alipata darasa huko la namna ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).


Rais Magufuli alipata darasa hilo ambalo linaanza kutekelezwa katika bajeti ya mwaka huu kutoka kwa Rais Paul Kagame ambaye shirika lake la Rwandair linatamba barani Afrika.


Dk Magufuli ametoboa siri hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa viongozi hao wawili wa nchi uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajia kununua ndege mbili mpya katika bajeti ya mwaka huu.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts