7/9/16

DC Kahama aanza kazi kwa mbwembwe

 
Mkuu mpya wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu amewazuia wakuu wa idara wa halmashauri tatu  kuingia kwenye kikao chake baada ya kuchelewa.
Nkulu aliwaita ofisini kwake wakuu wa idara wote wa halmashauri za Mji wa Kahama, Ushetu na Msalala kwa lengo la kujitambulisha na walikubaliana kikao hicho kifanyike saa mbili asubuhi ofisini kwake, lakini baadhi ya watumishi walifika zaidi ya saa mbili.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Anderson Msumba amenusurika kukumbwa na adhabu hiyo baada ya kuchelewa kwa sekunde chache.
“Wewe umefika saa mbili na sekunde moja, ingia wengine watakaokuja kuanzia sasa hawataingia kwenye kikao changu watakaa nje kusubiri,” amesema Nkulu.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts