Dudu Baya azungumzia aina ya mwanamke aliyenaye kwa sasa ‘kuna wakati ananishauri niache muziki’ | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

7/12/16

Dudu Baya azungumzia aina ya mwanamke aliyenaye kwa sasa ‘kuna wakati ananishauri niache muziki’

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Dudu Baya amesema mwanamke aliyenaye kwasasa hapendi suala la umaarufu na mara nyingi amekuwa akimshauri mambo mengi pamoja na swala kuachana na muziki.

Akiongea katika kipindi cha Uhondo kinachoruka EFM, Dudu Baya amesema mwanamke huyo ambaye kwa sasa ana ujauzito wake, ni mwanamke ambaye alianza naye mapenzi toka mwaka 2006.

“Kwanza ni mwanamke ambaye nimekutana naye tangu 2006, pili hapendi umaarufu na siku nyingi sana nimekuwa nikifanya interview nikawa ninasema mimi nataka mwanamke asinipende mimi kama Dudu Baya, anipende mimi kama Godfey Tumaini,” alisema Dudu. “Lakini kama una mwanamke alikupendea umaarufu, ukiondoka umaarufu na yeye anaondoka, kwa hiyo mpenzi wangu mimi hapendi vitu kama hivyo na sometime ananishauri niachane na muziki na nifanye biashara,”

Katika hatua nyingine Dudu Baya amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa kazi yake mpya ambayo inatoka wiki hii.

google+

linkedin