7/12/16

Gadner asema mkataba mnono umemrudisha Clouds FM, azungumzia mahusiano yake na EFM

Mtangazaji mkongwe nchini, Gadner G Habash, baada ya kurejea tena kwenye kituo chake cha awali, Clouds FM akitokea EFM, amefunguka na kuzungumzia maisha yake mapya ndani ya kituo hicho.
Gadner G
Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Gadner G Habash

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Gadner amesema kurudi Clouds FM sehemu ambayo alikaa kwa muda mrefu ni kitu ambacho kimemfariji sana.
“Maisha ni mazuri sana, ni maisha kama ukurasa mpya ambao nimeufungua,” alisema Gadner. “Namshukuru sana sana Mwenyezi Mungu amenipa kipaji lakini nawashukuru zaidi management ya Clouds FM kuona kwamba ninafaa nirudi pale tushirikiane tena, kwangu mimi naona ni kitu kikubwa japokuwa nilifanya kazi na Clouds FM kwa miaka 9 lakini bado hii nimeiona kama ni ukurasa mpya na nikitu kipya na ndio maana unasikia nasound kama mtu mpya,” alisema Gadner.
Pia mtangazaji huyo alizungumzia aliwezaje kurudi tena Clouds FM wakati tayari alishaanza maisha mapya na vituo vingine vya redio kama EFM.
“Ilikuwa ni vigumu sana kuondoka pale nilipokuwa (EFM) kwa sababu ya mazoea na urafiki ambao tulikuwa nao baina yangu mimi pamoja na staff ambao nilifanya nao kazi, baina yangu pamoja na viongozi, lakini wakati mwingine unapofanya uwamuzi, unahitaji kutumia hekima sana ili ufanye uwamuzi bila kuwa na hisia za kibinafsi, ufanye uwamuzi kutokana na nini biashara inataka, au ni nini maslahi yanataka na ndo utumie akili kuona kama maslahi yao. Zaidi ya hapo ujitahidi uondoke kwa mazingira yalio salama bila kukwazana na wale unaoachana nao, lakini ilikuwa ni ngumu, lakini kwa sababu Clouds FM walikuwa wananithamini kiukweli wamenipa offer ambayo ni kubwa sana na unajua wakati mwingine unamuomba mungu, lakini Mungu anakuletea bila kujua kama anakuletea nafikiri katika dua zangu ambazo nilimuomba Mungu aniongezee naona mkataba wangu mpya wa Clouds ameniongezea,”

chanzo: Bongo5
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts