7/4/16

Gondwe Awa Kivutio Uapishaji Ma-DC Tanga

ALIYEKUWA Mtangazaji wa ITV na Radio One, Godwin Gondwe, maarufu Double G, alikuwa kivutio kwa wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla ya kuapisha wakuu wapya mkoani humo.Gondwe ambaye mwishoni mwa wiki alikuwa miongoni mwa wakuu wapya nane wa wilaya za mkoa wa Tanga walioapishwa na mkuu wa mkoa huo, Martin Shigela, kushika wadhifa huo baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli, anakwenda kutumikia wilaya ya Handeni.

Umati wa wananchi walijitokeza kushuhudia tukio hilo na kusababisha ukumbi ilikukuwa ikifanyika hafla hiyo kuwa mdogo kutokana na wingi huo.

Hali ilidhihirika mara baada ya viongozi hao kuapishwa na kutoka nje ya ukumbi kwa ajili ya picha ya pamoja, ambapo kulizuka watu kukanyagana kila mmoja kutaka kuzungumza na mkuu huyo wa wilaya mpya na wengine kumpa mkono wa salamu.

Miongoni mwa wananchi waliyozungumza na Nipashe kuhusiana na uteuzi huo wa wakuu wa wilaya, Juma Shaban, alieleza kufurahishwa na Rais Magufuli kumteua Gondwe na kumpeleka mkoani hapa, huku akieleza matumaini yake kuwa wilaya ya Handeni itapiga hatua kimaendeleo kama ilivyokuwa alipokuwa mwanahabari mwingine, Muhingo Rweyemamu, alipokuwa mkuu wa wilaya hiyo.

“Handeni ilibadilika sana ilipokuwa ikiongozwa na Rweyemamu, Gondwe tulikuwa tunamuona ITV na kumsikia Radio One, sasa kawa mkuu wetu wa wilaya inatupa faraja kwamba atafanya vizuri kama ilivyokuwa kwa mwenzake,” alisema Mhando Mniga aliyedai kusafiri toka Handeni kuja kushuhudia hafla hiyo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts