7/12/16

Gwajima akamatwa na polisi

Jana mchana askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima amekamatwa Airport wakati akitua toka Nje ya nchi alikoenda kwa matibabu.
Duru za habari zinanyetisha kuwa Askofu Gwajima alishuka na ndege ya Kenya Airways iliyokuwa inatoka Nairobi kuja Dar ambapo baada ya kushuka alitaka kuunganisha na chopa yake kuingia mjini kupitia Sea Cliff.
Mpaka sasa Askofu yupo chini ya ulinzi na wafuasi wake na wasaidizi wake wamethibitisha kuwa walikuwa na taarifa za kuja kwa Askofu wao leo na ndege ya Kenya Airways lakini hawajamuona,na habari walizozipata ni kuwa mara baada ya kushuka vyomba vya Usalama vilimkamata sbb walikuwa wakimtafuta kwa muda mrefu.
Waumini wake na wasaidizi wake wanaendelea kufuatilia kujuwa kiongozi wao anashikiliwa katika kituo kipi cha polisi.Hizi habari zimezua "taharuki" kanisani kwake na waumini wapo katika makundimakundi kujadili hatima ya Askofu wao
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts