Gwajima: Leseni yangu ni ya Kuendesha Magari Makubwa | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

7/25/16

Gwajima: Leseni yangu ni ya Kuendesha Magari Makubwa

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemjibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtuhumu kuwa ni mwongo, akisema leseni yake ni ya kuendesha magari makubwa siyo vibajaji na maguta.

Akihubiri katika kanisa lake jana, Gwajima bila kutaja jina la Makamba, alisema: “Siwezi kushughulika na vigari vidogovidogo nyie mnanifahamu, nina leseni ya kuendesha semi trailer …nadhani mmenielewa,” alisema huku waumini wake wakimshangilia.

Juzi, Makamba aliwaeleza wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM kuwa, Askofu Gwajima ni kiongozi wa dini lakini ni mwongo na kuwa uongo huo unawaudhi hata waumini wake ambao ni wanachama wa chama hicho.

google+

linkedin