7/7/16

JPM ateua wakurugenzi halmashauri za majiji, wilayaRais John Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.
Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.
Wakurugenzi wote walioteuliwa wanatakiwa kufika Ikulu Jijini Dar es salaam siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 saa tatu asubuhi kwa ajili ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma. <<BOFYA HAPA>>
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm