7/2/16

JWTZ Kuendelea kutoa Ulinzi Mikoa ya Bahari
Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ limesema kupitia kikosi chake cha majini litaendelea kutoa ulinzi katika mipaka yote ya bahari ili kuzuia hatari zinazoweza kusababishwa na maharamia na watu wanaofanya uvuvi haramu wa kutumia mabomu.

Akizungumza mjini Mtwara,kufuatia ziara ya mitambo ya kuchakata gesi iliyopo madimba, Meja Jenerali Simon Mumwi wa jeshi hilo, ambaye ni mkuu wa mipango na maendeleo, aliyefuatana na maafisa wengine wa jeshi hilo, amesema kutokana na umuhimu wa nishati ya gesi na mitambo ya kuchakata nishati hiyo, iliyopo katika mikoa ya Lindi na Mtwara, Serikali imeona ni vyema kuongeza meli za kisasa za kufanya doria ya baharini.

Kwa upande wake,Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya TPDC, Dk. Shufaa Al Beity amesema Watanzania wanapaswa kuendelea kuwa walinzi wa mradi huo mkubwa wa uwekezaji katika nishati ya gesi na kuwa wavumilivu kuhusu maendeleo yatokanayo na nishati hiyo,

Serikali imenunua meli tano mpya za kijeshi ili kuhahakisha ulinzi unaimarishwa katika maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi katika mikoa ya Lindi na Mtwara, lengo kudhibiti uvamizi na uharibifu unaoweza kufanyika mitambo hiyo.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm