7/20/16

Kinana asema hakupenda kuwa katibu mkuu CCM

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Picha
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema nafasi hiyo hakuipenda sana lakini kwa kuwa aliombwa na wazee kuchukua nafasi hiyo ya utendaji mkuu wa chama alikuwa hana jinsi.
Kinana amesema kuwa amekuwa mtendaji wa CCM kwa miaka mitatu na nusu hivyo ni wakati wa kuondoka kama alivyoingia.
Alipoulizwa atafanyaje ikiwa ataombwa tena na Rais John Magufuli, amesema atafikiria na kuzungumza naye.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts