Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

7/26/16

Koffi Olomide akamatwa DR Congo

Mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amekamatwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.
Mwanamuziki huyo amekamatwa kwa agizo la ofisi ya mwendesha mashtaka wa DRC kufuatia tukio la kumpiga mcheza shoo wa kike katika nchini Kenya.
Olomide alitimuliwa kutoka Kenya baada ya video kuonekana kuonyesha akimpiga teke mcheza shoo wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mapema asubuhi baada yake kuwasili.
Alipangiwa kutumbuiza mashabiki wake Bomas of Kenya Jumamosi lakini tamasha hiyo ikaahirishwa.
Olomide alikamatwa Ijumaa usiku na maofisa wa polisi wa Kenya na siku iliyofuata asubuhi akaingizwa kwenye ndege na kurejeshwa Kinshasa.
Katika hatua nyingine, waandalizi wa tamasha ambalo Olomide alipangiwa kutumbuiza nchini Zambia pia walitangaza kufuta hafla hiyo kutokana na yaliyotokea Nairobi.
Mwanamuziki huyo, akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumapili, aliomba radhi mashabiki wake na hasa “wanawake na watoto”.
“Najutia sana yaliyotokea… kilikuwa ni kipindi kifupi cha wenda wazimu,” aliambia kituo cha televisheni cha taifa cha RTNC.
Baadaye, aliomba msamaha kutoka kwa raia wote wa DRC ambao huenda alihisi kwamba tabia yake iliwavunjia heshima.
Waziri wa masuala ya vijana na jinsia Kenya, Sicily Kariuki katika taarifa kwa vyombo vya habari baada ya video iliyoonyesha tukio hilo kusambaa, alipendekeza Olomide azuiwe daima kutembelea Kenya